Achana na Yaliyopita
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 2:1-3 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uweza wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Leo ni siku ya kuamkia Mwaka Mpya. Desturi ya wengi ni kusherehekea usiku wa manane tukiondokana na mwaka uliopita na kuingia mwaka mpya. Sherehe-sherehe. Lakini acha nikuulize, je! Mtu anaweza kuacha nyuma mwaka uliopita au bado unaweza kumtawala?
Hili ni swali nyeti, Ni mara ngapi tulitazamia mambo bora kwa mwaka mpya, lakini bado mapungufu ya zamani, kushindwa kwetu na hofu tuliyo nayo bado vinatawala fikra zetu na mioyo yetu.
Acha nikuulize tena. Je! mtu anaweza kuachana kabisa na yaliyopita? Kwa sababu hilo ndilo Mungu anataka ulifanye. Najuan kwamba hujakamilika. Bado una mapungufu yako, Na mimi pia niko hivyo. Lakini ruhusu Neno la Mungu –lililo hai na linalotenda kazi – liakuweke huru leo:
Waefeso 2:1-3 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uweza wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Cha kuzingatia katika mistari hiyo ni kuona kwamba yale yote yaliyoandikwa kwa wakati uliopita. Tulikuwa wafu katika dhambi zetu tulizoziendea. Sisi sote (hakuna anayekosa) tuliwahi kufuata tamaa ya mwili. Kwa asili tulikuwa watoto wa hasira.
Kesho nitakwambia habari njema, habari njema kabisa kuhusu hatima yako. Lakini kwa leo, tukubaliane hiki kimoja. Muda umefika wa kuachana na yaliyopita.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.