Chachu Kidogo …
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 5:6,7 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu.
Kinachonipendeza sana katika utamaduni wa Wayahudi ni namna wanavyotumia maneno kwa kuashiria mambo mbalimbali. Kwahiyo, kama umewahi kujiuliza kwanini chachu inatumika kama mfano wa dhambi kwenye Maandiko, basi tuangalie nini chachu au amira ina ashiria.
Mwili wangu haukubaliani vizuri na mkate, kwahiyo sili mikate mara nyingi. Lakini hali hiyo haiwezi kunizuia kusimama kidogo mlangoni mwa kiwanda cha kuoka mikate ili niweze kunusa harufu nzuri sana ya mikate iliyetoka jikoni.
Lakini pia, mikate inavutia sana unapoitazama dukani, Yaani kwa nje migumu lakini kwa ndani ni lainiiii, inaharufu nzuri sana lakini imevimbishwa na gesi iliyotoka kwenye amira.
Na ndiyo maana chachu ni alama ya dhambi kwenye Biblia. Ukiweka amira ndogo sana kwenye unga ya ngano, itasababisha uvimbe sana.
1 Wakorintho 5:6,7 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu.
Ndivyo kiburi kidogo kitakachofanya ndani yako – kitakuvimbisha sana. Kiburi hicho kitasabisha uonekane vizuri kweli kwa muda mfupi, lakini hatimaye utakuwa kama chakula kilichochina, kilichochacha.
Lakini mkate usiotiwa chachu, mkate wa Pasaka, au matza kama wanavyosema, haipendezi kwa macho, hainukii. Si mwepesi, yaani haina ufahari. Lakini ni mkate unaoweza kudumu muda mrefu sana bila kuchacha.
Kiburi hata kikiwa kidogo ni hatari sana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.