Cheche Ndogo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 3:3-5 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote. Tena angalieni merikebu; ingawa kubwa kama nini, na kuchuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha. Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Katika viiungo vya mwili, ulimi ni mdogo, haulingani na mkono au mguu, sindiyo? Lakini hata kama ni kadogo, unaweza kusababisha baraka tele au maumivu mengi.
Juzi, tulichunguza kwa pamoja Andiko hili:
Luka 6:45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Ina maana, kama vile Yesu ananukuliwa mara nyingi, ulimu hua unanena yaujaayo moyo wa mtu. Bila kuwa na moyo safi, bila kuwa na moyo ambao umeamua kumkaribia Yesu, kumwonea shauku na kutaka kumfuata, kumwabudu, kumtii … bila moyo wa namna hiyo, hakuna mema yanayoweza kumtoka.
Yakobo 3:3-5 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote. Tena angalieni merikebu; ingawa kubwa kama nini, na kuchuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha. Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majvuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Uzibiti ulimi wako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.