Dalili ya Mtu Aliyekua Kiroho
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:13-15 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo.
Swali. Hivi, anaonekanaje mtu aliyekua kiroho? Ni kipi kinachomtambulisha, au ni dalili gani inasababisha watu wengine wamtambue haraka kwamba yeye ni mkamilifu?
Nembo za magari kama Rolls Royce, Ferrari, Porsche zinajulikana haraka duniani. Ni kweli, wengi wetu na mimi nikiwemo, yawezekana hatuna uwezo wa kununua gari za fahari kama hizo, lakini hata hivyo, tunazitambua haraka.
Kwa hiyo acha niulize tena, je! Dalili ya mtu aliyekuwa kiroho ni ipi? Utawezaje kumtambua haraka? Mtume Paulo aliandika hivi:
Wafilipi 3:15 Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo.
Hii inaleta swali, je! Kuwaza hayo, ina maana gani? Jibu linapatikana kwa mistari michache iliyotangulia:
Wafilipi 3:13-14 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Kwahiyo, dalili ya mtu aliyekua kiroho si kwamba amekamilika kabisa, bali ni kule kukaza mwendo na kulenga kumaliza vizuri; bila kuangalia sana yaliyopita, bali kutumia nguvu zote kwa lengo la kufanana zaidi na zaidi na Kristo, siku baada ya siku.
Kama hili ndilo lengo lako, kama unajikaza katika lengo hilo hilo na kukubali kufundishwa na hata kurudiwa na Neno la Mungu, halafu ukaishia kanuni zile katika changamoto za maisha haya, lazima utakua kiroho.
Utaniruhusu nikuulize, je!, Umeshakuwa na utambulisho huo?
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.