... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Daraja la Kukufikisha Ng’ambo ya Shimo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 17:24 Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu; bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.

Listen to the radio broadcast of

Daraja la Kukufikisha Ng’ambo ya Shimo


Download audio file

Siku moja Mungu atafanya maajabu kupitia mimi, kweli kabisa! Atanituma huko au kule kufanya hiki na kile.  Ni ajabu.  Nina shauku kweli!

Je!  Umewahi kusema moyoni kwamba unataka kuutikisa ulimwengu huu kwa ajili ya Kristo?  kwa kutimiza kazi kubwa ya Mungu ambayo itawashangaza watu? 

Mimi ninakumbuka vizuri nilivyoota ndoto kama hizo na si vibaya kama hatuvuki mpaka.  Inatupasa sote kuwa na ndoto kubwa.  Si tunamtumikia Mungu mkubwa?  Amina? 

Lakini kuna pengo kubwa, au tuseme shimo kubwa katikati ya ndoto zetu kwa upande mmoja, na kuzifanya zitimie kwa upande mwingine.  Ni shimo ambayo wafuasi wengi wa Kristo wameshindwa kuweka daraja liwezalo kuwafikisha ng’ambo.  Wanaendelea kuota-ota na hatimaye ndoto zile zinachakaa. Hii ndiyo sababu ya Ndoto kufa bure: 

Mithali 17:24  Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu; bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia. 

Kama unataka ndoto zako zitimie kweli, inabidi utafakari kwanza yale ambayo yakupasa kufanya sasa hivi mahali ulipo.  Ni jambo gani linalopaswa nifanye kwa muda huu?  Ni akina nani niwashirikishe ambao wanao vipawa na vipaji mbali mbali vinavyotoka kwa Mungu?  Vitendeakazi vitatoka wapi, yaani uwezeshaji?  Tutaanzaje mipango hiyo? 

Lazima tufanye hayo yote kwa kutumia maombi na hekima ya ki-Mungu.  Lakini usifikiri kwamba Mungu atakutuma katika ncha ya dunia kama hujatumia hekima yake kwa yale ambayo yakupasa kufanya hapo hapo ulipo kwa muda huu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy