... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Huduma ya Kuwatia Moyo Wengine

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 12:25 Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; bali neno jema huufurahisha.

Listen to the radio broadcast of

Huduma ya Kuwatia Moyo Wengine


Download audio file

Inashangaza jinsi Mungu anaweza kutumia tukio la kawaida kutufundisha somo lenye nguvu, tukimruhusu, hata kama hatuko katika hali ya kiroho.  Hayo ndiyo yalinitokea hivi karibuni.

Nilikuwa kwenye mgahawa katika uwanja wa ndege wa mji wa Auckland nikisubiri ndege ya kunipeleka nyumbani.  Siku moja kabla ya safari, tulirecord vipindi 105 vya program yetu ya NENO SAFI LENYE AFYA kwenye studio ya TV.  Nilikuwa nimechoka mno.  Lakini nilikuwa nimekaa tu nikiangalia jinsi meneja wa mgahawa alivyoongoza watumishi wake.  Alikuwa kiongozi kweli! 

Cha kwanza niliona alivyokuwa anasaidia hapa na pale na kusafisha meza Baadaye alikuwa chap kumsaidia aliyekuwa anapokea malipo kwa sababu foleni ilikuwa kubwa sana. 

Ndipo niligundua.  Meneja huyu alikuwa na tabia nzuri na kuwatia moyo wafanyakazi wake. 

Mithali 12:25  Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; bali neno jema huufurahisha. 

Wahudumu kwenye mgahawa pale wangechanganikiwa kwa sababu ya kubanwa na kazi nyingi sana.  Lakini wote walikuwa wanatabasamu na kujali wateja.  Nilimshika yule meneja aliyeitwa Tim na kumpongeza na kumwambia kwamba ni kiongozi bora.

Uzito katika moyo wa mtu huimamisha; bali neno jema hufurahisha.  

Yule meneja Tim, kumbe alikuwa anaendesha huduma ya kutia moyo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.