... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Fursa Isiyowezekana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kutoka 33:12,13 Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Walakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu. Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako.

Listen to the radio broadcast of

Fursa Isiyowezekana


Download audio file

Kuna wakati Wakristo wanaweza kusema maneno ya ujinga, ni kweli.  Mfano, “Mungu hawezi kukuagiza kufanya jambo ambalo huwezi kulifanya.”  Hii ni kweli?  Watu hawa sijui wanaishi wapi?.

Ninakumbuka vizuri siku Mungu aliyoniita nimtangaze Kristo kwa watu ma-milioni. Kulikuwa na mwinjilisti mgeni aliyefika mjini kwetu. Alihubiri watu takriba kumi na moja elfu kwenye ukumbi. 

Maisha yangu yalikuwa yamechafuka.  Matumaini yangu na ndoto zangu zote zilikuwa zimeanguka chini.  Lakini hata hivyo, nilipoinua macho yangu na kuangalia umati ule wa watu, nilisema moyoni mwangu, “Laiti mimi ningeweza kuwaambia watu wengi hivi habari za Yesu, ingependeza sana.” 

Papo hapo nikamsikia Yesu akininongonezea, “Hawa ni wachache, fikiria watu ma-milioni.”  Ilikuwa haieleweki hata kidogo.  Yaani ilikuwa haiwezikani.  Je!  Hii ilikuwa fursa Mungu alikuwa anaiweka mbele yangu?  Kama ni fursa, basi ilikuwa fursa ambayo ingeshindikana.  Lakini kumbe, hayo yote si mambo mapya. 

Kutoka 33:12,13  Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami.  Walakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu.  Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. 

Musa hakujua hata kidogo namna atakavyoweza kuongoza Israeli kutoka Misri na kuingia Nchi ya Ahadi.  Lakini kama fursa Mungu anazoziweka mbele yetu zingekuwa zinawezekana, kama tungeweza kuzitimiza kwa nguvu zetu, basi, tusingemhitaji yeye.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy