... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hapana Neno Lililo Gumu Asiloliweza.

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yeremia 32:15,17 Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyumba na mashamba na mashamba ya mizabibu yatanunuliwa tena katika nchi hii ... Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza.

Listen to the radio broadcast of

Hapana Neno Lililo Gumu Asiloliweza.


Download audio file

Tunapaswa kukumbushwa kila mara, wewe na mimi, jinsi Mungu wetu alivyo mkuu na mwenye uweza. tunayokabiliana na mambo ambayo katika ulimwengu huu yanaweza kupunguza na kuharibu mtazamo wetu wa Mungu.

Bila shaka unajua inavyoenda.  Unakabiliana na shida kubwa maishani mwako, Halafu shida hiyo inaendelea kuweka kizuizi mbele yako na kuumiza moyo wako.

Kichwani mwetu tunaweza kuendelea kufikiri kwamba Mungu ana uwezo wote, kwamba yeye ni mkubwa kuliko shida zetu za ulimwengu huu na kuwa na mtazamo huo wa ki-Mungu ni vigumu mno. 

Taifa la Yuda lilikuwa limezingilwa na vita. Kilikuwa ni kipindi kigumu cha hatari.  Lakini Neno la Bwana lilimjia Yeremia, aende kununua shamba wakati wa vita kali.  Kwa nini? 

Yeremia 32:15  Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyumba na mashamba na mashamba ya mizabibu yatanunuliwa tena katika nchi hii. 

Yaani ilikuwa ni utabiri uliokuwa ngumu kuamini.  Lakini Yeremia aliendelea kuomba hivi … 

Yeremia 32:17  Aa!  Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza. 

Sasa dua yangu kwa ajili yako leo ni kwamba unabii huo, Neno hilo viweze kukutia ujasiri moyoni mwako leo.  Hajalishi mambo yakionekana kuwa vigumu kiasi gani, hakuna jambo lililo gumu asiloliweza kufanya Mungu.  Sisemi atalitenda kwa muda unaopenda wewe. Njia zake si kama njia zetu.. lakini kutenda, atatenda hakika. 

Wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lilile gumu usiloliweza.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy