Hekima Inayochanganya Watu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 1:20,21 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.
Sisi sote tunadhani kwamba tuna akili timamu; kwamba tunaweza kutafakari mambo na kuyachunguza ili tufikie maamuzi yaliyo sahihi.
Sasa kigezo hicho, karibia watu wote wana akili timamu, ndicho kinachofanya kwamba kesi zinazoweza kuamuliwa na baraza la wazee wa mahakama. Kwetu kikawaida raia kumi na wawili, wanaume na wanawake wanakaa pembeni ndani ya mahakama wakisikiliza hoja zinazoletwa na waendesha mashtaka na wanaomtetea aliyehutumiwa. Mwisho, baraza lile ndilo linaleta maamuzi kwa hakimu kwamba mhutumiwa ana hatia au ana haki.
Kuna watu baadhi ni wataalamu kabisa, wenye hekima katika taaluma zao, wanafalfasa, maprofesa, wanasheria. Lakini huwa inaweza kutokea kitu ambacho kinachanganya kabisa mantiki zao, hata sisi:
1 Wakorintho 1:20,21 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.
Jana tuliongelea habari za Msalaba jinsi inavyoonekana kuwa upumbavu. Kwa nini Mungu aliamua kumtuma Yesu kufa kwaajili ya jamaa kama wewe na mimi, ili atuokoe na mapungufu yetu … badala ya kutuhukumu moja kwa moja kuwa na hatia na kutuadhibu? Si ndivyo inavyoenda katika dunia hii?
Jibu: Ni kwasababu anakupenda sana kuliko namna ungeweza kuelezea. Ujue ukweli huo, ishi katika ujuzi huo, uwe kama pumzi kwako unayoivuta. Anakupenda zaidi ya namna ungeweza kufikiria, hata kama unakosea na kuharibu mambo.
Je! Ni upumbavu? Sidhani.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.