... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ikiwa Unaamini, Basi …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 2:19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.

Sijui kama ninaweza kukuuliza juu ya yale yaliyotokea wiki hii tunayoimalizia, je! Ni mawazo gani niliyokuwa nayo, ni maneno gani niliyoyatamka, ni mambo gani niliyoyafanya ambayo ninafahamu vizuri kwamba ni mabaya. Yakumbuke kwasababu tunataka kuyasimulia taratibu, wewe na mimi.

Kuna watu baadhi wanasema kwamba wanamwamini Yesu huku wakiishi maisha yanayotangaza utofauti kabisa.  Kwa upande mmoja wanajidai kuwa watakatifu, lakini kwa upande mwingine wanaishi maisha ya kashfa wakipotosha Neno la Mungu na kulipuuza. 

ninatumaini na ninaomba pia kwamba wewe uwe si mmoja wao, lakini tukisema ukweli, sote tunapungukiwa na utukufu wa Mungu; sisi sote wiki hii tu iliyopita tumefanya mambo yakutia aibu, na kwa kiwango fulani tumekuwa wanafiki – tukisema hiki na kutenda kingine. 

Sasa katika mazingira kama hayo, Mungu anayo ya kusema kupitia Mtume Paulo akimwandikia mwanafunzi wake kijana Timotheo: 

2 Timotheo 2:19  Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake.  Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu. 

Ni sehemu ya pili ya mstari huu nataka tulenge leo ili tuachane na unafiki na undumakuwili na kwa moyo wote, tujitakase, tukiwa watakatifu bila lawama ndani ya Kristo. 

Inatutia moyo kujua kwamba hicho ni kitu ambacho hatuwezi kukifanya kwa nguvu zetu – tena sio lazima tujaribu.  Kwa sababu kama umemwamini Yesu, una Roho wake ambaye tayari ameshakukirimia kwa nguvu zote zinazotakiwa ili ujiepushe na uovu. Kwa hiyo, katika mazingira kama hayo … pamoja na uwezo huo … tuache kutenda uovu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy