... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Injili Haiwezi Kunyamazishwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 2:3-6 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? Nao wakamwambia, Katika Bethelehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; kwa kuwa kwako atatoka mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli.

Listen to the radio broadcast of

Injili Haiwezi Kunyamazishwa

Download audio file

Kuna nguvu na mamlaka duniani ambazo zinatafuta kunyamazisha Injili, Habari Njema ya Yesu; kuwanyima watu wa Mungu wasipate nafasi ya kutangaza habari ya upendo ambao Mungu anaupenda ulimwengu.

Baadhi ya mamlaka hizo zinajifanya kuwa kama ni malaika wa nuru lakini kwa kweli ni nguvu za giza tupu, zenye mizizi ndani ya yule Mwovu anayetaka kuzuia watu wasiishi milele mbele za Mungu. 

Hayo nisemanyo ni yale yale Biblia inayofundisha.  Mapingamizi hayo yalianza miaka ma-elfu yaliyopita wakati Mfalme Herode alipojaribu kumuua Yesu akiwa bado mtoto mchanga. 

Mathayo 2:3-6  Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.  Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?  Nao wakamwambia, Katika Bethelehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; kwa kuwa kwako atatoka mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli. 

Inawezekana umeshajua yaliyotokea baada ya hapo, Herode alipojaribu kuendesha kwa hila wale mamajusi waliokuja kumwambudu Yesu; jinsi Mariamu na Yosefu na Yesu walipokimbilia Misri kabla ya Herode kuangamiza watoto wavulana ambao walikuwa chini ya umri wa miaka miwili kwenye nchi ya Wayahudi. 

Mamlaka ya uovu imejaribu kunyamazisha Habari Njema za Yesu Kristo tangu mwanzo kabisa. Lakini ni kazi bure Kwasababu – nisikilize vizuri – Habari Njema za Yesu hazitanyamazishwa kamwe wala haziwezi kunyamazishwa. 

Kwahiyo, hata ukikumbana na upinzani wa namna gani, usiogope kuwaambia watu habari za upendo wa Mungu ndani ya Yesu Kristo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy