... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hisia Yako Kali, Wito Wako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 15:16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

Listen to the radio broadcast of

Hisia Yako Kali, Wito Wako


Download audio file

Kama umewahi kujishughulisha na biashara ya matunda, kama mtu anayewajibika na kuzalisha matunda mema na kuyafikisha sokoni.  Basi hiyo ndio kazi waliyoitiwa wafuasi wa Yesu.

Unajua, wewe ni mtu wa kipekee sana, tena wa ajabu.  Kati ya watu mabilioni 8 wanaoishi duniani leo, na hata waliotangulia na watakaofuata, hakuwahi kuwepo mtu kama wewe, wala hayupo sasa na hatakuwepo. 

Ni dhana inayoshangaza na ya kufikiria na kutafakari sana. Wewe ni mtu wa kipekee kabisa!  Ina maana kwamba, unayo hisia kali kuhusu mambo kadhaa ambayo usingeweza hata kuyafikiria; pia kuna mambo unaweza kufanya ambayo sisi wengine hatuwezi kutimiza. 

Na kama unamwamini Yesu, basi jua neno hili: 

Yohana 15:16  Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. 

Akikujua kabisa jinsi ulivyo, hisia kali ulizo nazo na yale yote ambayo huna, Yesu amekuchagua – ndiyo, na amekupa kazi hii: enenda ukazae matunda, matunda na kukaa.  Mungu asifiwe kwa sababu matunda unayozaa wewe yatakuwa tofauti kabisa na matunda ninayozaa mimi. 

Kwahiyo, hisia kali ulizo nazo si za bahati nasibu, lakini ni wito wako.  Ukifuata hisia zile kwa jina la Yesu, kwa ajili ya utukufu wake, je!  Unafikiri itakuaje? 

Utakuwa ulimwenguni, ukizaa matunda yadumuyo milele katika maisha yako na katika maisha ya watu wengine.  Ndivyo ilivyokusudiwa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.