... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Katika Njia ya Haki

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 12:28 Katika njia ya haki kuna uhai; wala hakuna mauti katika mapito yake.

Listen to the radio broadcast of

Katika Njia ya Haki


Download audio file

Mara tena na tena, uchunguzi umegundua kwamba kampuni zinazoendelea kufaidika miaka nenda rudi, kwamba utendaji wao u katika maadili – yaani ni waaminifu, wanawatendea haki wafanyakazi wao pia wanajali wateja na kadhalika.

Zamani wakati mimi na wenzangu tuliokuwa tunafanya biashara kwa pamoja – wote tukiwa maofisa katika jeshi– tulianza kampuni yetu inayoleta ushauri katika mitambo ya teknolojia, tulimteua mtendaji wetu mkuu, mtu aliyekuwa na umri mkubwa na mwenye busara.

Na tangu mwanzo kabisa, aliweka bayana kanuni kubwa itakayoendesha kazi zetu zote, kwamba kila mara tutawashauri wateja wetu kwa faida yao tu, hata kama ushauri wetu usingetuletea faida katika biashara yetu.

Wakati ule sikuwa Mkristo, kwa hiyo iliniwia vigumu kuzoea kanuni hizo za maadili.  Lakini zilikuwa msingi wa mafanikio yetu kama kampuni.  Wateja wetu walituamini, na hii ilitupelekea kuzidi kupata kazi kwao na kwa wateja wapya ambao waliotuletea.

Majumlisho ya yote ni kwamba maadili hua yanaleta mafanikio.  Na hii isingetushangaza.  Ni dhana iliyokuwepa tangu nyakati za kale:

Mithali 12:28  Katika njia ya haki kuna uhai; wala hakuna mauti katika mapito yake.

Katika njia ya wema, njia ya haki, njia ya maadili mema, ndipo mtu atapata uzima, uzima wa kweli, uzima wa milele.  Kwa sababu gani?  Ni kwa sababu Mungu ni Mungu wa wema.  Yeye ndiye Mungu wa haki.  Kwa hiyo, tukiishi maisha yenye sifa hizo, tunakuwa tunaishi kwa mfano wake.

Jikague:  Je!  Kanuni zako za maadili zikoje siku hizi?  Je!  Dira yako inakupeleka wapi?  Kwa sababu … Katika njia ya haki kuna uhai; wala hakuna mauti katika mapito yake.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy