Kuachana kwa Talaka (2)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 19:8,9 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Mimi kama mtu aliyepitia maumivu ya talaka, nakwambia kwamba mtazamo wa jamii wa kisasa kuhusu ndoa unanishangaza sana, wakisema, “kinachopatikana kwa urahisi hupotea kwa urahisi”!
Tamaduni mbalimbali huwa zina mitazamo tofauti-tofauti kuhusu talaka. Lakini hata pale wanandoa wanapoachana kwa nadra sana, bado ndoa zile zinaendelea tu kisheria, lakini ki-matendo ni kama zimeshakufa kabisa.
Najua kuna wanaume baadhi ni wababe, Mungu anachukia ukatili. Pia kuna wake baadhi wamejitenga na waume zao kimwili na kihisa. Mungu anachukia tabia hiyo pia.
Halafu inawezekana kwamba kuna wakati lazima talaka iwepo. Wakati mwanamke na watoto wanaendelea kupigwa, lazima wakimbie. mke wa mtu anaendelea na tabia ya uasherati, hiyo ndoa haina budi kufutwa. Lakini mtazamo ule wa kusema, “kinachopatikana kwa urahisi, hupotea kwa urahisi” … kamwe haikuwa kusudi la Mungu. Na bado si kusudi lake. Wakati Yesu anahojiwa na viongozi wa dini kwanini zamani Musa aliruhusu talaka, Yesu alijibu hivi:
Mathayo 19:8,9 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Kama vile nilivyosema, kama hakuna namna, kama imeshindikana kabisa, hapo Mungu anaweza kuruhusu mume na mke kuachana. Kinachotuhuzunisha ni kwamba kule “kushindikana kabisa” huwa kunatokea mara nyingi kupita kiasi katika ulimwengu wetu. Lakini kama swala la uasherati halipo, kama hakuna ukatili wa mke na watoto kupigwa, kwa kweli ninyi waume na wake, nisikilize, Tumeagizwa kubaki pamoja, kuambatana kama mwili mmoja na kujitahidi kukarabati ndoa zetu.
Kwanini watu wanaachana na kupeana talaka? Sababu ya msingi ni kwamba hatutaki kupokea na kutii mafundisho ya Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.