... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kujidai Haki Haipendezi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 14:10-13 Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; na kila ulimi utamkiri Mungu. Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu. Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.

Listen to the radio broadcast of

Kujidai Haki Haipendezi

Download audio file

Leo, tabia ya kuhukumiana imekuwa kama ugonjwa wa kansa katika jamii.  Mtu akisoma kwenye mitandao ya kijamii dakika tano tu atagundua hilo. Si katika jamii tu. Hali hii ya kuhukumiana ni kansa ndani ya maisha yetu pia.

shutumu dhidi ya viongozi wetu na familia zao zinazotoka kwa watu ambao hawajawahi hata kutoa jasho kwa kuhudumia wengine ni mfano wa halisi wa ukosefu wa maadili na ni lazima lazima vikemewe. 

Lakini wewe na mimi tunafahamu vizuri kwamba kuna utofauti mkubwa kati ya kupima mambo bila upendeleo na tabia ya kuhukumu.  Mtume Paulo analo la kusema kuhusu tabia ya kuhukumu wengine:

Warumi 14:10-13  Lakini wewe je!  Mbona wamhukumu ndugu yako?  Au wewe je!  Mbona wamdharau ndugu yako?  Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.  Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; na kila ulimi utamkiri Mungu.  Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.  Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha. 

Swali la Paulo ni sahihi kabisa.  Mbona wamhukumu ndugu yako?  Kwanini tunakubali kushiriki tabia ya kuhukumu wengine tukijidai haki kama ulivyo mfumo wa kisasa?  Kwanini? 

Kama mtu mmoja alivyowahi kusema: Ujihadhari; kuondoa utu wa watu usiyekubaliana naye. Tunaposimamia haki zetu tunaweza bila kujua kuwa kama wale tunaopenda kuwakosoa.

Kwasababu kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.  Basi tusizidi kuhukumiana. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy