Kule Kuonea Shauku
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yeremia 27:7 Nimi nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni BWANA; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.
Kama unamwamini Yesu, bila shaka utakuwa umeshagundua kwamba mahusiano kati yako na Yesu kuna wakati yalipanda na kushuka. Kuna wakati yanawaka moto na kuna wakati yanapoa. Sasa kadiri kipindi kile cha kupoa kinavyokuwa kirefu ndivyo Yesu anavyoonekana kuwa mbali.
Mahusiano yetu na Yesu yanafanana na mahusiano ya kibinadamu. Ndoa inaanza na kiherehere cha mapenzi … halafu baada ya miaka kumi, mme na mke wakiwa wanalipa mikopo waliyochukua benki kwaajili ya kujenga nyumba, wakiwa na watoto wawili, wanaweza kuhisi kwamba wametengana sana.
Je, Upendo wa Yesu kwako Umepoa? La hasha – lakini kuna wahati huwa anasogea nyuma ili apime imani yako. Lakini sio shida sana kwa sababu yeye ni mwaminifu siku zote.
Lakini kama tutarudi nyuma zaidi na kuanza kuafikiana na dhambi ni sisi tunasogea nyuma, na kurudi nyuma zaidi na zaidi, na kuaanza kuafikiana na dhambi … hapo ndipo mioyo yetu inapoa na tunabaki kujiuliza kama kweli tunaweza kurudi kwenye mahusiano yale matamu tuliyokuwanayo awali. Je!
Mungu wetu ni mwaminifu. Kwahiyo, kama umerudi nyuma hatua fulani, sikiliza anavyokwambia:
Yeremia 27:7 Nimi nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni BWANA; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.
Kwahiyo Muombe abadilishe moyo wako ili uwe na shauku wa kumjua. Uombe Roho yake akushuhudia kwamba yeye ni Bwana wako. Halafu umgeukie kwa moyo wako wote. Anakuonea shauku kubwa na yeye ndiye awezaye peke yake kusababisha umuonee shauku tena.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.