... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumbatia Maisha Yako Mapya Leo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 2:1-5 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uweza wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakatu ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

Listen to the radio broadcast of

Kumbatia Maisha Yako Mapya Leo

Download audio file

Kama ulipata nafasi ya kunisikiliza jana, basi utakuwa unakumbuka kwamba niliahidi kukwambia habari njema inayohusu hatima yako.  Na hilo ndilo lengo langu leo.  Habari njema kabisa.

Sisi sote tumewahi kuanza mwaka mwingine mpya tukiwa na maazimio, matumaini na ndoto, lakini kama tukisema kweli, mengi yamekuwa yanafifia  tufikapo katikati ya mwezi wa kwanza tu, ahahaha 

Lakini mwaka huu utakuwa tofauti kwa sababu tumaini ninalotaka nikushirikishe si la kibinadamu, limetoka kwa Mungu. Uwezo unaenda kupokea si kitu ambacho unapaswa kutafuta ndani yako mwenyewe tu, bali unatoka juu mbinguni na huwezi kutuangusha. 

Waefeso 2:1-5 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uweza wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.  Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakatu ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. 

Mungu anataka uachane na yaliyopita.  Uwezo wa Neno lake ukuweke huru kabisa na yaliyopita.  Minyororo ya kale yavunjwe katika jina la Yesu. 

Hata kama ulikuwa mfu katika makosa yako, umehuishwa pamoja na Kristo.  Umeokolewa kwa neema ili uingie katika maisha mapya kabisa.  Kuishi maisha katika uwezo wa Roho yake. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy