Kupiga Hatua Kufika Kwenye Mwamba Imara
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 86:11 Ee BWANA, unifundishe njia yako; nitakwenda katika kweli yako; moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako.
Kwa kuwa sisi sote ni binadamu, mioyoni mwetu kuna mvutano kila mara kati ya nia ya kutenda mema na hali ya kushindwa na uovu. Si wewe na mimi tu!. Kila mtu anayekusudia kumfuata Yesu atakumbana na tatizo hilo.
Hua kuna mvutano moyoni mwako kati ya mema na mabaya. Unataka kutenda mema lakini kuna kitu kingine kinakushawishi sana. Na mtu hawezi kuendelea kuishi akiwa na moyo uliogawika. Hatimaye atapotoshwa. Akijua hivyo; Mfalme Daudi alitoa dua yake mbele za Mungu:
Zaburi 86:11 Ee BWANA, unifundishe njia yako; nitakwenda katika kweli yako; moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako.
Zamani, wakati nilipokuwa jeshini, tulijifunza vita. Walisema ni “michezo ya vita” ila haikuwa michezo ya kujifurahisha, Ilikuwa kazi ngumu, kuigiza mapigano ya aina zote za hali ya hewa – mvua, mvua ya mawe, thelugi, jua kali na kurudia-rudia mazoezi yale yale mpaka tufaulu kuyafanya vizuri.
Walimu wetu walitufundisha darasani kwanza nadharia ya kupiga risasi na mabadiliko ya mwendo lakini tulichoshwa mno wakati wa mazoezi tukiyarudia-rudia. Ndo maana ya “kufundisha” Inaashiria habari ya mpiga mishale akifanya mazoezi kwa kulenga – kitu mtu anaweza kufundishwa darasani miaka nenda-rudi, lakini ustadi wake unaotokana tu na mtu kushika upinde na mishale na kufanya mazoezi muda mrefu.
Kwahiyo, tunapomruhusu Mungu kutufundisha njia zake huko “kondeni” katika mapambano ya maisha haya, ndipo tunapozoea kuenenda katika kweli yake. Hatimaye utakuta kwamba moyo wako unaponywa na ule utengano uliokuwemo na maisha yako yatakuwa maisha ya kulicha jina lake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.