Kusameheana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 3:13 Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Hasira ni hisia inayoibuka mioyoni mwetu mara kwa mara pale tunapojisikia tumeonewa, sababu ni nyingi tu. Na huu ni muitikio wa kawaida kabisa.
Hata kama ni kawaida kwa mwanadamu kukasirika, kuna hatari kubwa mbili. Kwanza, mtu anapotawaliwa na jazba, anaweza kutamka maneno au kutenda mambo yanayoathiri kabisa na hawezi kuyarudisha. Pili, mtu akiruhusu hasira kuendelea kukaa moyoni mwake, itamkereketa na kupotosha mtazamo wake na kuharibu mahusiano yake na watu wengine.
Hata kama kuwa na hasira ni kawaida, mtu akiitumia kama silaha, kwa kweli inaleta uharibifu mkubwa. Sasa, unapomkasirikia mtu utafanyaje ili jazba isiendelee kupanda, utafanyeje ili upoe haraka bila kuleta madhara?
Wakolosai 3:13 Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Hii inawezekana kweli? Mkichukuliana. Ni neno rahisi kutamka, ila kulitendea kazi ni jambo gumu! … na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake. Sawa lakini hii ni agizo, lakini hatujasikia namna inavyowezekana. Mtu akikasirika, anahitaji kujua namnaya kufanya.
Ngoja nikuonyeshe namna ya kufanya: Kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Yesu alitoa uhai wake na damu yake pale msalabani wa ukatili ili wewe na mimi tuweze kusamehewa. La kufanya ukikasirika ni kuendea msalaba mara moja. Ni dawa kabisa ya kupoza hasira, kuleta utulivu ili na sisi tuweze kusamehe wengine. Hii ndiyo jinsi la kufanya, jambo ambalo daima tulihitaji kujua.
Kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.