... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuvumilia Tu … au Kushinda?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 8:35,37 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? ... Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.

Listen to the radio broadcast of

Kuvumilia Tu … au Kushinda?


Download audio file

Katika yote yanayotokea ulimwenguni bila kutaja shughuli za kila siku, wengi wanavumilia tu, wakipambana na maisha.  Lakini ingekuaje kama lengo la maisha ni zaidi ya kustahimili changamoto hizo?

Kwa kweli, mimi siwezi kufahamu kinachoendelea kwenye maisha yako muda huu, mema, mabaya, na yanayochukiza yanayoendelea maishani mwako unayafahamu wewe tu, Lakini pia na Mungu anafahamu yote. Lakini ujue kwamba, na Shetani naye anayafahamu kwa kujaribu kutumia madhaifu yako ili aweze kukuvuta mbali na Mungu na kukuangusha. 

Unapopambana na matatizo, pale Shetani anapovuruga hisia zako, unaweza kuhisi kwamba Mungu anazidi kusogea mbali nawewe. 

Lakini, unapojikuta kwenye hali kama hiyo, basi itakuwa muda mwafaka wa kuwa na mtazamo tofauti kabisa kwa kukabiliana na shida.  Kwa sababu hisia zetu sisi binadamu, huwa ni za kigeugeu, zikienda mbali na hali halisi ya mambo yanayokulenga wew: 

Warumi 8:35,37  Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?  Je!  Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? … Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 

Upendo wa Mungu una nguvu nyingi, ni wa kina kabisa tena ni amina kwamba hakuna kitu –kinachoweza kukutenganisha na upendo wa Kristo.  Si majaribu, shida, adha, njaa, uchi, hatari, au upanga.  Hakuna! 

Na kwa sababu ya upendo huo mkubwa, Kristo anataka ushinde hisia zako, ushinde tatizo ulilo nalo, ushinde kile kitu kinachokusumbua, si kukivumilia tu kwabababu wewe ni zaidi ya mshindi kupitia YEYE anayekupenda.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy