... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwekwa Huru mbali na Dhambi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Tito 2:11-14 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.

Listen to the radio broadcast of

Kuwekwa Huru mbali na Dhambi

Download audio file

Mimi ninaona kama kuna hatari pale mtu anapoelewa vibaya maana ya neema ya Mungu – ni kama anajenga uzio kwa kuzunguka dhana hiyo moyoni mwake na fikra zake hata kusababisha asione uwezo wa neema ya Mungu katika kubadilisha maisha yake.

Kuna sababu kubwa za mtu kuzuia uwezo wa neema ya Mungu maishani mwake.  Huwa nikuanza kufikiri kwamba lengo kuu na pekee la neema ya Mungu ni kutusamehe tu.  Lakini hii si kweli. 

Ni kweli kwamba neema ya Mungu inatuletea msamaha pale tunapoweka tumaini letu kwa Yesu aliyelipa gharama za deni la dhambi zetu pale msalabani.  Lakini bado kuna mengine mengi.  Ebu tuyachunguze kidogo: 

Tito 2:11-14  Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. 

Umesikia vizuri?  Ni kweli, tunaokolewa kwa neema ya Mungu.  Hakuna mjadala.  Lakini neema ile inatufundisha kuishi kwa hekima, kwa njia sahihi na  kumcha Mungu pia. 

Neema ya Mungu ni uwezo wa kubadilisha maisha yetu.  Neema haiwezi kutusamehe dhambi tu, bali inatuweka huru na dhambi.  Hayo ni mapinduzi makubwa katika maisha ya mwanadamu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy