... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Lakini Sielewi!

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 11:8,9 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

Listen to the radio broadcast of

Lakini Sielewi!


Download audio file

Mzazi yeyote anafahamu namna inavyokatisha tamaa pale anapomwambia mtoto  wake kufanya jambo fulani na yeye kuitika kwa kudai, “Kwa nini afanye?!” kama sharti kabla ya kutii.  Kuna wakati kuna jibu linalohitajika kwa swali lake na wakati mwingine hamna.

Ukweli ni kwamba huwezi kuweka kichwa cha mzee juu ya mabega ya kijana. Baba yangu aliniagiza kusafisha chumba changu kila jumamosi asubuhi na  mama alinisisitiza kufanya mazoezi ya kupiga kinanda angalau nusu saa kila siku (mambo yote mawili yalinichukiza enzi zile) wasingaliweza kunielezea matunda ambayo yangetokana na nidhamu hizo ndani ya tabia yangu baada ya miaka mingi. 

Hali kadhalika, kuna wakati Mungu anatuagiza kufanya mambo tusiyopenda; mambo yasiyoeleweka; mambo tisiyotaka kuyafanya hata kidogo. Sasa kipindi kama hicho, ndipo imani inatakiwa itende kazi au la. 

Waebrania 11:8,9  Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.  Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 

Mungu aliwaita Ibrahimu na mke wake Sara kutoka kwenye maisha ya starehe na anasa kwenda kwenye safari yenye mashaka, safari isiyowezekana, safari yenye usumbufu kwa kipindi cha miaka ishirini na mitano. Hawakujua kamwe mahali Mungu anapowaelekeza lakini walianza safari kwa imani; walimtii Mungu tu; pasipo kuelewa. 

“Imani” ni kufuata na kumtii Mungu, hata kama haieleweki. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy