... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ni Swala la Moyoni

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 11:4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akashuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

Listen to the radio broadcast of

Ni Swala la Moyoni


Download audio file

Labda umesikika wanavyosema kwamba pasipo imani haiwezikani kumpendeza Mungu.  Ni kweli.  Maneno hayo yametoka moja kwenye Neno la Mungu, yaani kwenye Waebrania 11:6.  Lakini, lina maana gani hasa kwenye maisha yetu ya kila siku, hmm?

Mimi daima ninajaribu kuelewea Neno la Mungu kwa kulilinganisha na hali halisi ya maisha.  Kwasababu, kama mtu ana nia ya kumwamini Yesu na kumfuata (hatua itakayomgharimu bila shaka ni kupata majaribu); atapenda kujua namna yale anayoyapitia yanavyoweza kuleta mabadiliko mazuri na yenye maana kwenye maisha yake, amina? 

Sasa, kwa mistari inayotangulia juu ya pale tuliponukuu – pasipo imani haiwezikani kumpendeza Mungu – Bwana anatupa mfano hai unaoweza kutusaidia kuelewa maana ya msatari wa sita. 

Waebrania 11:4  Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akashuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena. 

Sasa, Kaini na Habili walikuwa wana wa Adamu na Hawa.  Hatimaye, Kaini alimwua ndugu yake Habili kwasababu ya wivu, kwa kuwa Mungu alizipokea sadaka za Habili lakini hakupokea sadaka za Kaini.  Kwanini Mungu alipendezwa na sadaka za Habili na akizikataa za Kaini? 

Ni kwa sababu Habili alitoa sadaka yake kwaimani akiamini kwamba Mungu ni mwema, bali Kaini alikuwa anatoa kwa mazoea tu kwa sababu alikuwa na uovu moyoni uliodhihirika pale alipomuua mdogo wake. 

Kama wewe unajikuta unafanya mambo kwa mazoea tu, ni muda mwafaka wa kubadilika moyo wako, kwa sababu pasipo imani haiwezikani kumpendeza Mungu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.