... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Fumbo Kubwa la Imani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 11:1,3 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana ... Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyo-onekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

Listen to the radio broadcast of

Fumbo Kubwa la Imani


Download audio file

Kutokana na nadharia ya sayansi wanasema, vitu vyote vilitokana na “mripuko mkubwa” uliotokea miaka ma-bilioni yaliyopita. Lakini ni nani aliyeandaa tukio lile na ni kipi kilichosababisha mripuko?

Hayo ni maswali ambayo sayansi haiwezi kujibu hata kidogo.  Mtu hawezi kuweka nadharia kuhusu maswala kama hayo … haiwezikani. Dhana ya kwamba kitu kimetokea tu kwa hali ya kutokuwepo kitu haieleweki.  Kwa mtazamo ya sayansi, itaendelea kuwa ni kitendawili tu. 

Lakini kwa Mungu kuna jibu.  Hapo mwanzo Mungu aliziumba … aliumba kila kitu kutoka utupu. Inabidi tujiulize, kwanini wewe na mimi inatuwia vigumu kuamini kwamba Mungu angeweza kufanya hiki au kile; kwamba anaweza kushinda kisichowezekana; kwamba anaweza kuhamisha milima; kwamba anaweza kukidhi mahitaji yetu pale tunapokuwa na ukosefu mkubwa!? Kwa nini tuna mashaka? 

Siku hizi tumejaribu kufafanua ukweli wenye nguvu kwamba imani hata kama ikiwa ndogo sana kama punje ya haradali, bado inaweza kusababisha vitu vitokee. Sikiliza nenola Mungu linavyosema: 

Waebrania 11:1,3  Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana …  Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. 

Hata kama huwezi kuona kitu au huwezi kukieleza ama kukigusa, hizo sio sababu za kusema hakipo. Usihofu kupiga hatua ya imani na kuingia kwenye mpango ya Mungu. Kwasababu imani yako, hata kama ni ndogo, hata kama haijakamilika, inayumba-yumba, bado itasababisha mipango ya Mungu itokee.  Tumeshirikishwa katika ushirikiano wa ajabu katika kazi za Mungu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.