Maana Halisi ya Ufalme
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Wakristo wanaongea sana kuhusu “Ufalme wa Mungu”; yaani wanautamka kwa urahisi. Sana, Lakini tutafakari kwanza. Hivi tunaelewa kabisa maana yake? Je!, Tuko tayari kukubali maelezo ya ufalme?
Siku hizi, wafalme wachache wanabaki wakitawala nchi zao, kwa sehemu kubwa, wanashika nafasi ile kama nembo, madaraka yao ya kweli yakiwa madogo sana kulingana na katiba za nchi zao. Lakini Yesu alikuwepo hapa duniani, mfalme alikuwa na madaraka kabisa juu yao, alikuwa hata na mamlaka ya kuamua aidha waendelee kuishi au wauawe.
Ilikuwa hivyo katika historia ya Israeli, na ndivyo ilivyokuwa chini ya Kaisari wakati taifa linatawaliwa na Warumi. Kwa hiyo, Yesu alipoongea habari ya “Ufalme wa Mungu”, alikuwa anaeleza habari za mamlaka ya mwisho ya mwenye madaraka. Kwa hiyo, tusome mstari ufuatao tukiwa na uelewa huo:
Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Ina maana, badala ya kufuatilia sana yale yote tunayotamani katika maisha haya (na kweli kuna mambo mengi sana ya kutamaniwa) inatubidi wewe na mimi, kuwa na shauku hasa kwa Ufalme wa Mungu; utawala wake wenye amri zote peke yake; kumtii na kufanya yale anayotaka yeye. Je! Uko tayari kuyaweka kuwa kipaumbele chako … au la?
Mwalimu wa Biblia aitwaye Glenn Bleakney alieleza hivi: “Kuna watu baadhi wanataka kumtendea Mungu kama vile Mfalme Sauli alivyomtendea Daudi; wanataka aue majitu na kufukuza pepo wachafu, lakini asitawale kama Mfalme!”
Kumfuata Yesu ni kutubu, kuachana na dhambi zako, kumruhusu Roho wake akubadilishe ili unapotafuta utawala wake maishani mwako uwe na kipaumbele, utakuwa na uwezo wa kumtii. Je! Hayo ndio unayoyataka kweli?
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.