... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Krismasi Mwezi wa Saba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.

Listen to the radio broadcast of

Krismasi Mwezi wa Saba


Download audio file

Inategemeana mahali unapoishi, lakini swali ninaloenda kukuuliza labda litaonekana kuwa la tofauti kabisa. Je!, Umewahi  kusherehekea Krismasi mwezi wa saba?  Sitanii. Umewahi kusherehekea Krismasi mwezi wa Julai, yaani mwezi wa saba?

Kwa kuwa Krismas ni mwezi Disemba, huku kwetu tunapoishi nusu ya dunia Kusini mwa ikweta ni majira ya joto sana. 

Kwahiyo, kuna migahawa baadhi ifikapo mwezi Julai (ambayo ni majira ya baridi kwetu) wanaandaa mlo mkuu rasmi wa Krismasi ya Mwezi Julai, wakitengeneza aina zote za chakula kama yalivyo mapokeo ili tuweze kutumia mlo ule majira ya baridi. Ni kweli hata kama utashangaa. 

Jambo hilo lilinisababisha kutafakari sana. Kwanini tunasherehekea ujio wa Mwana wa Mungu hapa duniani siku chache mwisho wa Desemba?  Kuna mchungaji maarufu akiwa pia mwalimu wa Biblia aitwaye John MacArthur alisema hivi: 

“Watu wengi wanapenda kufurahia kuzaliwa kwa Kristo wakati wa Kirsmasi tu, lakini wanampuuza na kumkataa siku zingine katika mwaka.” 

Ni kweli kabisa.  Ni wangapi wanaenda kanisani mara moja tu kwa mwaka, siku ya Krismas?  Je! Hii inapaswa kuwa mwisho wa habari?  Akitabiri kuhusu Yesu karne nyingi kabla ya kuzaliwa kwake, Nabii Isaya aliandika hivi: 

Isaya 9:6  Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. 

Hmm. Mimi naona kama kuja kwa Yesu –  Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani – ni tukio ambalo latupasa kusherehekea kila wakati.  Kwa hiyo, acha nikuulize tena, je!  Umewahi kusherehekea Krismasi mwezi wa Julai? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.