... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwaonekania Wenye Shida

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:12,13 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Kuwaonekania Wenye Shida


Download audio file

Nadhani ninaweza kusema kwa uhakika kwamba, wewe na mimi, tuna watu tunaofahamiana nao, ambao sasa hivi wako wanapitia vipindi vigumu. 

Na mara nyingi, usibishe tafadhali, sisi tunalenga mambo yetu tu, tukiwa bize sana na “yale makuu” yanayotupasa kufanya, kwahiyo, hatuna muda tena wakuwatembelea wale wanaosumbuliwa na mambo magumu. 

Wakolosai 3:12,13  Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 

Mimi naona kama huruma, fadhili, unyenyekevu, upole na uvumilivu wa kuchukuliana mizigo vinachukua muda wa kutosha.  Tunahitaji kuwa na moyo wa kujali wengine.  Mwanatheolojia aitwaye Paul Allen, akiwa pia mwandishi aliandika hivi: 

“Kwenye Kipindi kigumu, mtu hataki kuambiwa ajipe moyo na kuangalia yaliyo mema tu, bali anatakiwa kujua kwamba uko upande wake.  Hata kama huwezi kumsaidia kupona, bado unaweza kumsaidia ajue kwamba anaonekana. Njia bora ya kutegemeza wengine, si kuwatia moyo kwa maneno, bali ni kuwatembelea.” 

Je!, Ni yupi katika wale unaowafahamu, anapitia kipindi kigumu muda huu?  Je!, Ulichukua nafasi ya kusimama kwanza, kumwangalia, kumwona, kumwendea na kusimama naye japo kidogo?  Ni jibu sasa,Umeyafanya? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.