... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mahusiano ya Wasiwasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 13:4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

Listen to the radio broadcast of

Mahusiano ya Wasiwasi


Download audio file

Ukichunguza dunia ilivyo leo, tukiwa na mitambo na vyombo vinavyoshikika mikononi na vyenye uwezo mkubwa kuzidi kompyuta kubwa za zamani, imekuwa rahisi sana watu kutokuwa waaminifu tena kwa ndoa zao na kuanguka katika uasherati.

Ni msiba mkubwa sana mno, mtu anakuwa na mahusiano yasiyofaa, anaangalia picha chafu kwenye mtandao , hayo yote yanavunja ndoa. 

Waebrania 13:4  Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. 

Nikisoma mstari kama huo, ninapenda kuchunguza nielewe maana yake zaidi.  Mwandishi akisema, “malazi yawe safi”, anamaanisha kwamba wanandoa wawe waaminifu kabisa kwa ahadi zao. 

Ni rahisi kukataza na kusema … usithubutu kuzini!  Lakini si rahisi kujibu swali linalofuata, Mtu atajilindaje? Mtu afanyeje katika ulimwengu wetu huu ambao picha chafu zinatujia kama mafuriko kila wakati, atafanyaje asianguke ndani ya mtego wa jaribu la namna hiyo? 

Jibu: ni kwa kuheshimu ndoa yake. Kuhakikisha kwamba ndoa imejaa urafiki wa ndani kihisia na kimwili pia kama vile Mungu alivyokusudia tangu mwanzo.  Ebu kubumka kwamba ndoa ilikuwa wazo lake mwanzoni tena ameifanya kuwa baraka kwa mume na mke. 

Msinyimane. usimezwe na matumizi ya simu yako hadi uka haribu ndoa yako.  

kutokujali mwenzi ni kutokuheshimu ndoa. Uwe makini hapo, kwasababu lazima ndoa iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. 

Waume na wake … heshimuni ndoa zenu na za watu wengine, Msinyimane bali ili msianguke ndani ya jaribu na kuhukumiwa adhabu na Mungu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy