Maisha ya Uzima Tele
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 3:16-19 Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
Kuna utofauti mkubwa kati ya maisha ya uzima tele na maisha tupu, maisha yanayobariki wengine na yasiyobariki , maisha ya kuridhisha kabisa na maisha ya mahangaiko tu. Je! Wewe unaishi maisha gani?
Ni swali linaloleta tafakuri kwa kweli kwa sababu mtu anaweza kuendelea na shughuli zake za kila siku , hatimaye akazeeka, asiwe tena na shughuli nyingi, pengine akiwa na upweke ,yaani maisha yanaendela tu bila mwelekeo hadi yanaisha.
Hatimaye, mtu akikaribia mwisho wa maisha yake, ndipo anagundua kwamba hakuishi maisha ya uzima tele kama alivyotadhania.
Yesu aliahidi kwamba watu watakaomwamini bila shaka watateswa kama yeye alivyoteswa. Haya ni maneno mazito, lakini pia aliahidi kwamba tungeishi maisha ya uzima tele. Kuna mtu mmoja aliniuliza maana ya kuishi “maisha ya uzima tele.” Nilimjibu kwa kutumia maneno ya Mtume Paulo wakati alikuwa anaelezea rafiki zake.
Waefeso 3:16-19 Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
Maisha ya “uzima tele” ni maisha ya kuwa na nguvu ya undani, Kristo akikaa moyoni mwa mtu, maisha yenye shina na msingi katika upendo, maisha katika upana ule wote wa wingi wa pendo lake Mungu kwetu. Kwa hiyo niulize tena, je! Unaishi maisha ya aina gani?
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.