Ujumbe Ulio Wazi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 15:33,34 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu.
Lazima nikwambie, Mtume Paulo ananipendeza sana. Yaani hakwepeshi neno – anasema bila kuficha. Tukisoma yale aliyoyaandika, hatuwezi kutatanishwa hata kidogo kwa kutokuelewa maana yake.
Kusema ukweli, mimi nimemuelewa vizuri Mtume Paulo kwasababu ninafanana naye. Kule kusema wazi kwangu kunaumiza watu baadhi, lakini sina budi kufanya hivyo. Na leo sitasita, yaani ni siku ya kuweka mambo bayana.ahahahaha
Kama tumefuatana kwenye kipindi hiki wiki hii, unajua ya kwamba tumechukua muda wa kutosha kuchunguza sura moja ya Biblia inayoeleza habari ya ufufuo – 1 Wakorintho 15. Ni sehemu nzuri kuchunguza, ikitueleza kwanini yatupasa kuamini habari za kufufuka kwa Kristo. Na bado tutaendelea kujifunza.
Lakini katikati ya hoja zake, anaenda pembeni kwa kutoa ujumbe mfupi unaogusa sana, kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, ujumbe muhimu sana. Huu ndio ujumbe huo mfupi:
1 Wakorintho 15:33,34 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu.
Sijawa na ujasiri kuwaandikia rafiki zetu wanaotuunga mkono kwenye huduma yetu kwa lengo la kuwaaibisha. Lakini humo humo ndani ya Biblia tunaona ndivyo alivyofanya Paulo. Kwanini? Ni kwasababu katika sura hii inayohusu ufufuo, Paulo anaingiza onyo kali. Anachokisema ni kwamba kama wewe au mimi tutaendelea kutenda dhambi, tutapoteza ahadi ya uzima wa kuishi milele pamoja na Yesu.
Bila kuficha ujumbe wake unasemaje? Acha kutenda dhambi!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.