... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu Hashindwi Wala Hachoki

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Hoseya 2:13-15 Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA. Kwa hiyo angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo. Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.

Listen to the radio broadcast of

Mungu Hashindwi Wala Hachoki

Download audio file

Hivi umewahi kujikuta unagaa-gaa kwenye matokeo ya makosa yako huku ukijiuliza utapitia wapi kupatoka?, Ni njia ipi utamrejea Mungu kwa utimilifu?

Kweli, sehemu kama hiyo haipendezi, lakini kila mmoja hana budi kupapitia mara kwa mara. Sote tumekula matokeo mabaya ya makosa yetu, makubwa kwa madogo. Sote tumechapwa na fimbo ya nidhamu ya Mungu – Kama vile baba mwema yeyote ni lazima atawarudi wale anaowapenda. Sasa tukifikia mahali hapo, lazima tujiulize, Je! Kuna njia ya kurejea kweli? 

Katika historia ya Israeli, kuna wakati hawakuwa waaminifu kwa Mungu (kama tabia yao ilivyokuwa).  Katika Agano la Kale kwenye kitabu cha Hosea, Mungu anawafananisha na kahaba, aliyepotea katika ukahaba wake. Je inawezekana mtu atoke katika hali kama hiyo? 

Hoseya 2:13-15  Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA.  Kwa hiyo angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo.  Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri. 

Angalia ajabu hii! Mungu atamfanyaje kahabu huyo Israeli?  Atamshawishi na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo; atampa mashamba ya mizabibu; 

Tuweke wazi kabisa. Mungu hachoki wala hashindwi kukurejesha. Yeye mwenyewe ndiye njia ya marejesho.  Yeye ndiye mlango wako wa tumaini. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.