Neema Iletayo Ujasiri
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 4:14-16 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo wetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Haya, ninakutakia Krismasi njema na yenye furaha, Siku maalum katika mwaka tunachukua nafasi kukumbuka namna neema ya Mungu ilivyoingia ulimwenguni kupitia Mtoto yule aliyelazwa horini.
Lakini kwa watu wengine huu umekuwa mwaka mgumu sana, inawezekana mtu akajisikia kama amepigwa vibaya na maisha kiasi ambacho inamwia vigumu hata kuinua macho yake juu na kumshukuru Mungu kwa kumtuma Yesu duniani kwa ajili yake.
Isitoshe, kila mmoja wetu anaweza kuangalia nyuma na kukumbuka makosa yake na upungufu aliyokuwa nayo kwa mwaka mzima, na kama akijiona kama hafai mbele za Mungu hali hiyo inaweza kumsababishia mtu asiweze kusherehekea vizuri ujio wa Mwokozi Yesu, si kweli?
Kama ndio hali yako basi nina habari njema kabisa kwako. Habari hii inaeleza ni kwanini Yesu alikuja duniani kwa ajili yako:
Waebrania 4:14-16 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo wetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Kwasababu Yesu alipitia njia hii hii ya uanadamu, njia ya mateso basi anatuelewa vizuri sana. Na kwa sababu hiyo, sasa leo hii, wewe na mimi tunaweza kuja mbele ya kiti chake cha neema kwa ujasiri ili tupewe neema na kugundua upya neema yake wakati wa mahitaji yetu. Hii ndio Krismasi na ndivyo Yesu alivyo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.