Nimeharibu – Sasa Nifanyeje?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 15:17-19 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
Ni lini uliwahi kuona aibu kwasababu ya tendo ulilolifanya? Si hisia inayopendeza, au? Kama vile Adamu na Hawa kwenye Bustani ya Edeni, mwelekeo wetu tukikosea ni kwenda na kujificha Mungu asituone.
Ni kweli kabisa, aibu inakufanya utake kufunika uso wako. Maana, ni nani angependa kila fikra mbaya, kila kosa, kila jambo la uovu alilolifanya, kama vingebadilishwa kuwa picha zilizobandikwa sokoni ili wote wavione? Yaani kama ni wewe, sidhani ungethubutu kuonekana tena kwenye maeneo hayo.
Labda unaufahamu mfano wa Yesu kuhusu mwana mpotevu, kijana aliyeasi, akachukua urithi wake na kuondoka na kutapanya mali yake yote kwa maisha ya ufisadi. Wakati anafilisika, alianza kuhangaika – jambo ambalo halinabudi kutokea tukimwasi Mungu. Lakini hatimaye …
Luka 15:17-19 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
Alibadilika pale njaa ilipozidi, aibu ya kurudi kwa baba yake na kukiri makosa yake. Kama unafahamu habari hii, unajua kwamba baba yake alimpokea kwa shangwe.
Uamuzi ule wa kurudi ni mapambano. Kwahiyo, kama unaona aibu na ukiwa na mivutano moyoni, jua kwamba dini inasema hivi: Nimekosea vibaya, baba ataniua, lakini Injili inasema: Nimekosea vibaya, lazima nimbipu baba.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.