Samehe Bila Kuadhibu
Add to FavouritesWakolosai 3:13,14 Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Kuna njia nyingi sana ya kuonyesha upendo kwa watu wanaotuzunguka. Ni kipaumbele kwenye agenda yake Mungu kwa ajili ya maisha yako na maisha yangu. Mtu Atafanya nini wakati mahusiano fulani yameishavunjika?
Ni swali linalokusumbua, si kweli? Fikiria juu ya mahusiano uliyekuwa nayo ambayo leob hii yameshaharibika kabisa. Jaribu kukumbuka kidogo, sura ya mtu yule mliyekorofishana , na alikuwa mtu wa karibu, inaumiza zaidi, sindiyo?
Kwa moyo wangu wote, ninajua kwamba Mungu anataka kukuweka huru na hisia zile mbaya – hofu, hasira, na hali ya kutokusamehe inayokulemea. Sikiliza sasa:
Wakolosai 3:13,14 Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Msamaha. Ni funguo inayoweza kukuweka huru pia madhaifu sehemu kubwa au ndogo kwa binadamu wote. Sasa mtu akitoka kwenye hali ile ya uchu wa kumwona kuwa binadamu mwenzake aliyekosea, kidogo-kidogo, hasira itapungua na kumfungulia njia ya kumsamehe.
Labda utaniuliza, “Kwanini nifanye hivyo?” Ni kwa sababu Bwana amekusamehe na ilimgharimu uhai wake. Kwa hiyo … Mchukuliane, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.