Tayari Ameshakubariki Sana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo.
Ni jambo lisiloepukika kwamba tukilinganisha mwaka uliopita na kutazama mwaka mpya ulioko mbele yetu, tunatazamia kwamba mambo mengine yataboreka. Yatatengamaa na kutuletea baraka.
Sasa, mambo unayotamani yaboreke maishani mwako ni yapi? Je! Ni mibaraka gani unatamani kuipata?, Bila shaka unaweza kutaja moja au mawili yenye muhimu kwako.
Labda ungependa mambo yaende vizuri zaidi kazini, kwenye uchumi, kwenye ndoa, kwenye maisha ya watoto, yaani, orodha haina mwisho, sindiyo? Kwa hiyo, mara nyingi, tunalenga baraka ya kwanza au hata ya pili tu; ambazo hatujajaliwa kupata kana kwamba nyingine hazina umuhimu sana.
Hii ni kawaida, hasa kwa majira haya, wakati mtu anajikagua na kutazamia kwamba yaliyo mbele yatakuwa bora. Hii ni sawa, lakini kuna hatari kwamba mtu akilenga yale ambayo hajapata, atakosa kuona kabisa yale yote aliyoyapata
Waefeso 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo.
Ukweli ni kwamba ndani ya Kristo, tayari Mungu ameshatubariki kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho. Alitukuta sokoni pale wanapouza watumwa, akatununua na kutukomboa kwa damu ya Yesu, Ametusamehe kwa sababu Kristo alilipa deni. Ameweka Roho yake ndani yetu na kutuweka kwenye njia inayotupeleka mahali tutakapoishi mbele zake milele.
Ukweli ni kwamba ndani ya Kristo, tayari Mungu ametubariki sana sana – wewe na mimi. Kamwe usisahau ukweli huo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.