Unafiki wa Wakristo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 3:6-9 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
Ni lini mtu alikwambia kitu ambacho kilikuchoma, kilisababisha ushtuke, Jaribu kukumbuka,
Nina jirani yangu ambaye daima ana maoni hasi, kila anaponiona anakuwa tayari na maneno ya kunichokoza.Uutashangaa nikikwambia kwamba ninafurahi nikiweza kutoka kwetu au kuingia tena nyumbani bila kukutana naye.
Ni maneno yapi wewe na mimi tunayotoa na kuwatamkia Wengine wanatuonaje baada ya kutusikia? Na zaidi ya yote, Mungu anawaza nini?
Yakobo 3:6-9 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum. Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu. Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
Ndivyo ilivyo, si kweli? Kwa kuvuta pumzi tu, sisi ambao tunajiita Wakristo tunamhimidi Mungu, lakini kwa kuvuta pumzi tena, twawalaani wanadaamu Mungu aliyeumba kwa mfano wake, watu ambao anawapenda.
Ulimwengu unamchukia mnafiki. Sidhani kwamba Mungu anapendezwa na wanafiki. Angalia sana yale unayoyasema.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.