... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usitende kwa Hasira

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 37:8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.

Listen to the radio broadcast of

Usitende kwa Hasira


Download audio file

Acha nikuulize, Ni kipi kinasababisha hasira yako ipande mara kwa mara?  Kila mtu ana vitu vinavyoweza kumchokoza akasirike na tunapokuja juu adrenalini inazidi kuzunguka ndani ya mishipa yetu ya damu na hapo tunaweza kufanya mambo ya kipumbavu kabisa.

Labda wewe ni mmoja wa watu wenye bahati ya kuwa na asili ya upole, kwa hiyo swala la hasira halikusumbui.  Kama uko hivyo, basi, Mungu akubariki.  Lakini mimi binafsi niko tofauti. Nilizaliwa nikiwa na hisia kali kwenye damu yangu ya kutenganisha haki na yasiyo haki.  Sasa mtu anapovuka mipaka na kutenda yasiyo haki, kusema ukweli mara moja ghadhabu huwa inapanda ndani yangu. Kwahiyo, zoezi la kudhibiti hasira yangu ni changamoto kweli. 

Labda umeshasikia wanavyosema, eti, ukikasirika, hesabu kwanza moja hadi kumi kabla ya kuitika. Lakini kama vile binti mmoja aitwaye Lucy alivyosema: ukihesabu moja hadi kumi, utakuwa umedhamiria kutenda jeuri! 

Kwahiyo, hata kama una tabia gani, utafanyaje pale mtu anapokuchokoza vibaya? 

Zaburi 37:8  Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya. 

Katika mstari huu mfupi, kuna vitenzi vitatu vyepesi lakini vyenye nguvu – maneno yanayoashiria utendaji.  Kukomesha hasira – ni kulegeza na kuachilia (nadhani huo ndio mfumo wa kuhesabu kwanza moja hadi kumi). 

Pili, ni kuachana na matendo yanayoendana na ghadhabu na hasira yako.  Kuacha kabisa nia ya kujilipiza kisasi.  Maana yake ni kuondoka pale. 

Mwisho, usikasirike, kwa maneno mengine, usiache hasira iendelee kuwaka chinichini kwa sababu ukiiruhusu, matokeo yake ni kutenda mabaya. 

Yamkini, hukusikia vizuri, kwahiyo nitarudia mstari: 

Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly