... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wakati Mtu Anaishiwa Kabisa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

Listen to the radio broadcast of

Wakati Mtu Anaishiwa Kabisa


Download audio file

Je! Umewahi kuwa na aibu kwasababu una kidogo tu cha kuchangia kwa mahitaji ya watu wengine, na kama wewe ni mtu wa imani, unajisikia vibaya kwasababu huna ya kutosha kutegemeza kazi ya Mungu?  Wengine wanaweza kutoa mengi kabisa, lakini mimi sina.

Labda wewe ni tajiri na swala la kutoa kwa ukarimu halijakusumbua.  Au pengine wewe ni kama mimi mtu ambaye amepitia hali ngumu hata kukosa pesa za riziki sembuse kuwa na za kuweka kwenye sadaka jumapili.  Nakwambia, hali hii inasababisha mtu kujisikia vibaya sana. 

Nilikumbushwa vipindi vigumu kama hivyo nilipoguswa sana na maneno ya mchungaji wa kanisa letu aitwaye Stuart Crawshawa, maneno aliyoyasema wiki iliyopita. Si kila mtu atajikuta katika hali ambayo inamuwezesha kutoa, lakini kila mtu yupo sehemu ambayo anaweza kuomba. 

Jamani!, ni mara ngapi tunavyowaza kwamba maombi tu hayawezi kufaa kuchukua nafasi ya kuomba?  Mara nyingi tunaweza kufikiri kwamba kwa kusema “Nitakuombea” ni kutafuta udhuru tu lakini kusema ukweli maombi na maombezi ni zoezi lenye nguvu sana kwenye misheni kuliko huduma zote zingine. Kwasababu kupitia maombi ni kama tunakuwa bega kwa bega na Mungu kwa kuhakikisha kwamba mapenzi yake yanafanyika hapa duniani. 

Lakini usinikubalie kwa matamshi yangu tu. 

Yakobo 5:16  Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa.  Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. 

Ni kweli kabisa kwamba lazima tupambane na dhambi maishani mwetu.  Ni kweli kabisa kwamba lazima tuwe na msimamo sahihi mbele za Mungu kupitia imani yetu ndani ya Yesu. Lakini matokeo ni yafuatayo:  kwamba kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.  

Kamwe usipuuze uwezo wa maombi yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy