... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wito wa Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 16:10,11 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli?

Listen to the radio broadcast of

Wito wa Mungu


Download audio file

Mtu yeyote aliyekusudia kumfanyia Mungu kitu anafahamu namna mwanzo unavyokuwa mgumu sana. Lakini kadiri mambo yanavyotengamaa ndivyo yanavyozidi kuwa bora, mafanikio yanaanza kuonekana huko mbeleni. Hapo ndipo kuna hatari kabisa.

Niliambiwa siku hizi habari ya dhehebu fulani iliyoweza kumlipa mhubiri maarufu dola za kimarekani $150,000 kuhudumia mkutano wao wa siku moja tu!, ni balaa!, lakini dhehebu hii kama zingine, ilianzishwa zamani na watu wachache ambao walikusudia mioyoni mwao kumtumkia Mungu. 

Yaani, mafanikio yanauwezo wakupotosha makusudi mema tunayoweza kuwa nayo ya kumtumikia Mungu. Si kwa huduma zile zinazochukua muda wote wa watumishi, bali ni katika sekta zote za maisha yetu. Kwasababu mafanikio yanaleta kiburi kichwani, yanapotosha maamuzi yetu kuliko kuzidi tulivyokuwa mwanzoni mwa huduma zetu.

Lakini Mungu anaona yote haya. Sasa sikiliza onyo la Mungu linavyotujia moja kwa moja kutoka kwa Yesu mwenyewe: 

Luka 16:10,11  Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.  Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? 

Uwe mwaminifu kwa mambo madogo. Mama Teresia aliwahi kusema hivi, “Mungu hajaniitia mafanikio.  Bali ameniita niwe mwaminifu.” 

Rafiki yangu, ujue kwamba Shetani atajaribu kukuangusha kwa njia mbalimbali.  Kwahiyo, mtazamo wako usipotoshwe, usidanganywe na mvuto wa mafanikio katika huduma.  Uwe mwaminifu tu – kwa madogo na kwa makubwa pia.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy