... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Achana na Majuto

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:12,13 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo ...

Listen to the radio broadcast of

Achana na Majuto


Download audio file

Muda huu, wengi wetu tunaanza kutathmini mwaka unaoenda kuisha … Je!  Uliendaje?  Je!  Ulikuwa mwaka mzuri au mbaya?

Vipi?  Umeendaje?  Ulifaulu mwaka huu?  Je!  Umekamilika zaidi?  Umetimiza malengo yako au la?  Haya yote yanagusaje hisia zako ukitafakari mwaka mpya unaokuja? 

Usishangae.  Kwa kweli nina maswali mengi leo, lakini nina nia njema kwa sababu Mungu yu pamoja na wewe katika maswali hayo yote.  Yeye anataka ahusishwe katika mambo yajayo, ili akuongoze na nguvu zake katika mipango aliyokuandalia.  Sasa, ni muda mwafaka kwetu kumwacha aongee nasi kuhusu mwaka unaoenda kwisha na jinsi tunatazamia yatakayotokea mwaka mpya. 

Wafilipi 3:12,13  Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la!  Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.  Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo … 

Huyu ni Mtume Paulo akitathmini yaliyopita katika maisha yake na kutazama yaliyopo na kutazamia yatakayokuja.  Ukweli ni kwamba hakuna aliyekamilika.  Sote tunakosea.  Sisi sote bado kuna mengi twapasa kujifunza.  Kwa hiyo jaribu kusahau yaliyopita ili ukaze mwendo ufikie lengo ambalo Mungu ameweka mbele yako,  Kwa sababu maluum 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.