... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ahadi Zake ni za Kweli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 18:30 Mungu, njia yake ni kamilifu, ahadi ya BWANA imehakikishwa, yeye ndiye ngao yao wote wanaomkimbilia.

Listen to the radio broadcast of

Ahadi Zake ni za Kweli


Download audio file

Swali: Je!  Mungu ni wa kutegemewa?  Unajua, ametoa ahadi nyingi sana katika Neno lake.  Zingine zinaonekana kuwa za ajabu-ajabu katika pirika-pirika za maisha.  Je!  Ni za kutegemewa?  Je!  Yeye mwenyewe anaweza kuaminiwa?

Katika karibia sekta zote za maisha, kuna nadharia yake na kuna utendaji wake.  Mtu anaweza kujifunza nadharia fulani mpaka anachoka kabisa, lakini haiwezi kumsaidia wakati mambo yanapamba moto. 

Wakati nilikuwa jeshini, ilibidi tufanye mazoezi ya kuigiza jinsi ya kushambulia adui mara kwa mara.  Ni sawa tu, ila hatukuwa na risasi za kweli ndani ya bunduki zetu.  

Nakumbuka jinsi nilivyofikiri wakati ule, je!  Ingekuwaje kama ingekuwa vita ya kweli?  Je!  Ingekuwaje kama risasi za kweli ndizo zingepita juu ya vichwa vyetu?  Ingekuaje kama ningeona rafiki yangu aliye pembeni yangu kupigwa risasi shingoni?  Je!  Nadharia ya kupigana vita itafanya kazi wakati ya vita ya kweli?  Ndivyo ahadi za ajabu za Mungu zilivyo.  Haziwezi kukuhakikishwa hadi zimepimwa katika vita inayopamba moto. 

Zaburi 18 iliandikwa na Daudi, Mfalme wa Israeli kama wimbo wa kumwimbia Mungu, siku Bwana alimwokoa mkononi mwa adui zake wote, akiwemo yule aliyetaka kumwua, yaani Sauli: 

Zaburi 18:30  Mungu, njia yake ni kamilifu, ahadi ya BWANA imehakikishwa, yeye ndiye ngao yao wote wanaomkimbilia. 

Hayo ni maneno ya mtu aliyepitia mengi.  Hayo ni maneno ya mtu aliyejaribisha ahadi za Mungu katika vita, wakati uhai wake ulihatarishwa.  Ni kweli, kuna wakati Mungu anaweza kutuongoza hatarini. Lakini njia yake ni kamilifu, ahadi ya BWANA imehakikishwa, yeye ndiye ngao yao wote wanaomkimbilia.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.