... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Iwe Nuru

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 5:14-16 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Listen to the radio broadcast of

Iwe Nuru


Download audio file

Kuna mara maisha inakuwa kama kitendawili.  Yaani yale yote yanayoendela maishani mwako, moyoni mwako, katika familia yako, pale unapoajiriwa … mara ingine hayaeleweki kabisa.  Kinachohitajika ni kupata mtu ambaye angeleta mwangaza juu ya yote, ili nuru iweze kukusaidia kuelewa kinachoendelea.

Kama wewe ni Mkristo, unajua mambo mazito yanavyoweza kuvunja moyo ukizingatia kwamba tunaamini kwamba Mungu ana uwezo wote, kwamba upendo wake haupimiki.  Ni Mungu anayetawala juu ya vyote, akitamalaki kila sehemu. 

Lakini fikiria ingekuaje kwa mtu asiyemjua Mungu, mtu ambaye hajapata mwangaza wa upendo wake moyoni mwake?  Hawa ndiyo Mungu ametutuma kwao kama vile tochi kumulikisha nuru yake katika giza iliyomo mioyoni mwao.

Yesu alielezea watu wa kawaida; wakulima, wenye maduka, vibarua wala si viongozi wa dini waliokuwa madarakani; maneno yafuatayo:

Mathayo 5:14-16  Ninyi ni nuru ya ulimwengu.  Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.  Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.  Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Kwa hiyo, rafiki yangu, kama unamwamini huyu Yesu aliyekuwa nuru ya ulimwengu na hata sasa bado ni nuru ile ile, ujue hili:  Amekuteua kuwa kama taa yake, uweze kuwaangazia wengine.  Kwa mafupi, wewe ni nuru ya ulimwengu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.