... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Utaamua Kupumzika?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 11:28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Listen to the radio broadcast of

Je! Utaamua Kupumzika?


Download audio file

Ni ukweli kinzani au tuseme ni kitendawili, kwamba hata wakati mtu anapumzika vya kutosha – akipata usingizi vizuri na burudani baada ya kazi – bado anaweza kujisikia kwamba hana raha, bado anachoka.  Kuna sababu hali hiyo hua inatokea.

Mwili kupumzishwa ni sehemu moja tu ya swala la mtu kupata raha.  Ili apumzishwe kabisa kabisa, nafsi yake lazima itulie, ipumzike.  Yaani lazima moyo wake uwe na amani.

Hauna budi kukutana na vipingamizi.  Bila shaka kutakuwa mahusiano ambayo yatasumbua.  Kutakuwa mivutano na fadhaa kuhusu hiki au kile.  Asubuhi ile, wakati nilikuwa ninaandaa kipindi hiki cha leo, nilifahamu vizuri yaliyonikabili siku ile kwamba ilinilazimu nitatue tatizo gumu katika taasisi yetu.  Maisha ndivyo yalivyo.  Hua inatutokea sisi sote. 

Na ni katika mazingira hayo hayo, akiongea na watu kama sisi, Yesu aliweza kutamka hivi:

Mathayo 11:28-30  Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.  Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Wakati tunapambana na maisha haya, tukibeba mizigo inayotulemea, Yesu anatoa aliko.  Anatuita, akitualika leo hii katikati ya harakati za maisha, tuje kwake.  Kwa nini?

Ni kwa sababu yeye peke yake ndiye awezaye kutupa raha nafsini mwetu.  Ndiyo maana wengi sana hawajapata mapumziko halisi.  Ni kwa sababu wanapuuza wito wake.  Je!  Wewe utamwitikia?  Je!  Wewe utaamua kupumzishwa?

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.