... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mashtaka ya Shetani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ayubu 1:10-12 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Mashtaka ya Shetani

Download audio file

Katika Neno la Mungu, Shetani anaitwa Ibilisi na Mshitaki.  Lakini je!  Umewahi kufikiri kwamba angeweza kuthubutu kumshitaki Mungu?  Kwa kweli alifanya hivyo zamani wakati wa Ayubu!

Je!  Shetani alimshitaki Mungu kwamba alifanya nini?  Sikiliza jinsi Shetani alivyoongea moja kwa moja na Mungu: 

Ayubu 1:10-12  Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo?  Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.  Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.  BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe.  Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA. 

Je!  Shetani alimshitaki Mungu nini?  Kulinda na kumbariki Ayubu; kumfanikisha katika shughuli zake zote.  Kwa kweli Shetani alishitaki kwamba Mungu amemzingira Ayubu na ukigo usiopitika pande zote. 

Mimi nadhani kwamba swali lililo muhimu zaidi la kuuliza tukisoma Andiko fulani ni hili:  Je!  Linanifundisha nini kuhusu Mungu?  Hapa, linatufundisha kwamba Mungu ni Mungu anayetulinda.  Kumbuka jana tuliona kwamba malaika zake Mungu hua wanapiga kambi ya ulinzi kwa kuzungukia watu wake. 

Ni kweli, kuna mara Mungu anaweza kuondoa ule ulinzi ili apime imani yetu kama alivyofanya kwa Ayubu.  Lakini kumbuka jinsi Yesu alivyofundisha wanafunzi wake kuomba.  Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. 

Maneno hayo ndiyo ninayoomba kila siku.  Siombi kwamba Mungu aniongezee nguvu ili nimshinde Shetani, bali ninaomba Mungu asababishe akae mbali nami. 

Mungu akulinde na akubariki pia. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.