... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Unaweza Kupanda Mlima Ule Mrefu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:23,24 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Unaweza Kupanda Mlima Ule Mrefu


Download audio file

Je!  Ni lini ulipowahi kukabiliana na mlima mrefu kiasi ambacho ulionekana kwamba mtu hawezi kuupanda?  Je!  Unakumbuka jinsi ulivyotishiwa?  Jinsi ulijua kwamba isingaliwezekana kabisa?

Mwezi Mei 2016 mtu ambaye namheshimu sana alinijia na kuniambia: “Nafikiri Mungu amekuita uanze kipindi cha Neno la Mungu cha televisheni cha kila siku.”  Mara moja niliamua kwamba ni jambo ambalo lisingewezekana.  Nilitoa udhuru za kila aina, nikimwonyesha kwamba haiwezekani … lakini tulipomaliza masimulizi yetu, kumbe!  Ndani yangu ilisikika sauti ndogo ikiniambia kwamba ndivyo inavyonipasa nifanye.

Sasa, baada ya miaka saba na nusu, leo hii, tarehe mosi ya mwaka mpya, tumefikia ujumbe wa 2,500 wa Neno la Mungu Safi na Lenye Afya.  Ni ratibisho ya mawazo elfu mbili na mia tano, machapisho na kurekodi redio, kushuti TV … kipindi kimoja kimoja. 

Si kwamba nataka kujisifu, hapana; bali nataka nikutie moyo nikikwambia ukweli huu, kwamba … ili mtu apande mlima mrefu, lazima achukue hatua ndogo moja baada ya ingine.  

Wakolosai 3:23,24  Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi.  Mnamtumikia Bwana Kristo. 

Bila shaka, Bwana ameandaa jambo lisilowezekana ili ulifanye, jambo likupasalo kulianza.  Lo lote lile amekuonyesha, lifanye kwa moyo, lifanye kwa ajili ya Bwana, hatua moja baada ya ingine.  Kwa sababu hatimaye thawabu yako itatoka kwake.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.