... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Utajiri Wake Katika Utukufu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 4:19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu

Listen to the radio broadcast of

Utajiri Wake Katika Utukufu


Download audio file

Katika ulimwengu huu unaozidi kutajirika, inatuwia vigumu zaidi kutenganisha matamanio yetu na mahitaji yetu.  Mara nyingi, hasa wakati tunaomba, tunachanganya hayo mawili.

Hapa ninapoishi, karibia watu wote wanaona kwamba kuoga maji moto kwenye bafu kuwa haki ya msingi ya kibinadamu.  Je!  Mtu angewezaje kuamka na kuanza kufanya shughuli zake bila kuoga maji moto?

Huu ndio ulikuwa mtazamo wangu hadi pale nilipokutana na umaskini kijijini Halia nchini India.  Pia, wakati nilitembelea kituo cha wenye ukoma Tanzania na kutoa miche ya sabuni mikononi mwa watu ambao hawakuwa tena ni vidole.

Mambo hayo yanamsaidia mtu kupambanua kati ya mahitaji na matamanio.  Lakini bila kushtukiwa kwa kushuhudia hali duni la watu baadhi, ninajiuliza kwamba mara nyingi tunamwendea Mungu tukimsihi kututimizia haja fulani la msingi (kama tunavyofikiria sisi) lakini kwa kweli kile tunachokiongelea kumbe ni matamanio yetu tu.

Mtume Paulo aliweza kutenganisha vizuri sana kati ya mahitaji na matamanio yake wakati aliandika maneno yafuatayo akiwa gerezani akisubiri hukumu ya kifo:

Wafilipi 4:19  Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Kwa kweli, Mungu bado anajishughulisha kabisa na zoezi la kukidhi mahitaji ya watu wake.  Kumbuka, Paulo alikuwa amefungwa mnyororo.  Hatimaye aliuawa.  Sasa yuko mbele zake Mungu milele daima.

Hata sisi tunaweza mara kwa mara, kujikuta tumefungiwa ndani ya jela aina fulani.  Hapo hapo Mungu atakidhi tele kila hitaji letu.  Si kama bahili bali kwa ukarimu, sawa sawa na utajiri wake katika utukufu.  Ndivyo alivyo Mungu.  Lakini kamwe tusichanganye hata mara moja, mahitaji yetu na matamanio tuliyo nayo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.