Haina Makona Mengi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 4:8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
Watu wanasumbua, si umeshaona? , kuna wengine wanasumbuana sana, sana! Soi hivyo tu, kuna wakati wanatutendea vibaya tena kwa makusudi. Sasa, ni mara ngapi tumejitahidi kuwaonyesha fadhili na upendo, hmmm?
Wengi wetu na mimi nikiwemo, tunaishi kwa kasi tukiwa bize sana. Najua si wote wanaoishi hivyo. Lakini hata kama wewe una tabia ya upole, ukaishi taratibu-taratibu, bado ni rahisi kuishi kwa ubinafsi na kutokujali ustawi wa wale wanaokuzunguka.
Na mimi ninataka kuwa muwazi. Kuna kipindi kwenye maisha yangu niliwatendea watu waliokuwa karibu yangu kama si binadamu na huku nikiendelea kuwa na shauku kubwa ya kumtendea Mungu mambo makubwa.
Popote ulipo, haijalishi unaishi kwa kasi gani au umefikia hatua gani katika maisha yako au kuwa na mtazamo wa namna gani, Leo ni muda mwafaka wa kujitathmini.
1 Petro 4:8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
Ni muhimu sana kuliko yote unayoweza kufanya … uwe na juhudi nyingi katika kupendana. Hata wale wanaokuumiza au kukusumbua, kwasababu upendo huo utasitiri wingi wa dhambi. Upendo huo utakuletea uponyaji, tumaini, saburi na amani.
Mwandishi akiwa pia mwalimu aitwaye Amy Klutinoty, alijumlisha hayo kwa kusema hivi: “Kama kumpenda mtu anayesimama mbele yako kunaonekana kuwa huduma finyu machoni pako, ni kwasababu umesahau unyofu wa Injili, kwamba haina makona mengi.”Ni sahili kabisa.
Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.