... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hautapotea

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 10:29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

Listen to the radio broadcast of

Hautapotea


Download audio file

Kuna jambo baya mno ambalo linaweza kumpata mtoto mdogo, ni kutengwa na wazazi; kupotea; yaani kifungo kile cha usalama kuvunjika hata kama ni kwa muda mfupi.

Ninakumbuka nilipokuwa mtoto mdogo jinsi nilivyopotea katika duka kubwa la nguo. Yaani pale walipotundika nguo kwenye enga palikuwa ni parefu sana kwangu na kuzuia nisiwezi kuona. Sikuweza kumwona mama yangu.    

Kwa wakristo wengi, hofu ya kupotea, huwa inaweza kuinuka mara kwa mara.  Itakuaje nikienda mbali?  Itakuaje nikikosea vibaya pale Mungu atakaponiacha? Itakuaje kama Shetani atanivuta na kunipeleka kwenye uharibifu?  Itakuaje? 

Nisikilize. Kama uliwahi kuweka tegemeo lako kwa Yesu, unaweza kuwa na uhakika thabiti wa mambo mawili:  Kwanza, haikutokana na wewe mwenyewe, ilikuwa ni kazi ya Mungu.  Pili, hakuna uwezo wo wote katika viumbe vyote unaweza kutangua mapenzi yake. 

Usinikubalie mimi kama mimi.  Sikiliza alivyosema Yesu mwenyewe: 

Yohana 10:29  Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. 

Ni kweli, kama kondoo yoyote, mtu unaweza ukapotea na kwenda, Lakini Mchungaji Mwema ataacha kondoo wengine tisini na tisa na kwenda kukutafuta. Atakutafuta kweli na kukurejesha nyumbani.

Hakuna mtu au uwezo wowote katika viumbe vyote vyneye uwezo wa kukupokonya kwenye mkono wake. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.