... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hisia, Shauku, Mihemuko

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 40:7,8 Majani yakauka, ua lanyauka; kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani. Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele.

Listen to the radio broadcast of

Hisia, Shauku, Mihemuko


Download audio file

Maoni ya watu wengine, hususani wakiyatetea kwa nguvu (kama vile wanavyofanya siku hizi) yanaonekana kama yanazomea na kuzima ukweli wa Neno la Mungu, hadi imani ya Mkristo wa kawaida inaanza kufifia.

Kuna sababu kubwa huwa inatokea, ni kwamba, uovu, uchoyo na mambo mengine mengi ambayo siogopi kuyaita kama yalivyo … dhambi, imekubalika na kuwa kawaida katika jamii hata kutukuzwa, kwa sababu, Shetani anajifanya kuwa malaika wa nuru. 

Na hali hii imetikisa sana Mkristo wa kawaida. Juzi nilisoma yafuatayo, sijui ni nani aliyeyaandika, lakini ni huzuni kukiri kwamba anayoyasema yanazidi kuonekana kuwa ya kweli: 

“Tumefikia mahala katika Ukristo, ambapo watu hawajali kama mtu anaweza kutetea oni lake kwa msingi wa Biblia.  Bali hisia, shauku na mihemuko ndivyo vinavyopuuza na kutangua yale Maandiko yanayoyasema.  Yaani hawafuati Kristo, bali wanafuata mambo yao binafsi.” 

Kwahiyo, naomba uniwie radhi kwa swali hili, Je!, Ni kwa kiwango gani kule kufanya dhambi kuwa kawaida katika jamii kumekupotosha uende mbali na kweli ya Neno la Mungu na uwezo wake?  Kwa sababu … 

Isaya 40:7,8  Majani yakauka, ua lanyauka; kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake.  Yakini watu hawa ni majani.  Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele. 

Angalia, Neno la Mungu ni kweli hata kama viwango vya maadili katika jamii vimeporomoka, hata kama tunakubaliana nalo au la. 

Najua sio rahisi kusimama imara. Hautakuwa na starehe wala kupendwa na watu. Lakini pokea tahadhari hii.  Shetani anatujia akivijika kuwa na hali ya malaika wa nuru. Usidanganywe.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.