... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hofu ya Mauti

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 5:6-8 Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.

Listen to the radio broadcast of

Hofu ya Mauti


Download audio file

Wengi wetu hatupendi kuwaza sana kuhusu kifo. Ndiyo, kwa upande mmoja, tunajua hakika kwamba siku moja tutakufa. Lakini kwa upande mwingine, hatutaki siku hiyo ifike.

Sisi sote tunapambana na swala hilo na kadiri tunavyozidi kupata mvi na ngozi kupata kunyanzi, ndivyo dhana ya kifo inazidi kuzunguka katika fikra zetu.  Siku niliyoandaa somo hili, nilikuwa najiandaa kwenda kumuona mama yangu hospitalini. Ana umri wa miaka 92 na jirani yake alikuta ameanguka chini jikoni siku moja kabla. 

Ukizingatia umri wake na jinsi afya yake inavyozidi kuzorota, mimi nina uhakika kwamba , mama anatafakari sana habari za kifo kuliko kukuzidi wewe na mimi. Kwahiyo, kama hofu ya kifo inakusumbua kwenye mawazo yako, basi pokea neno hili litokalo kwenye Neno la Mungu, neno linalolenga tatizo lako:

2 Wakorintho 5:6-8  Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.  (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)  Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. 

Yaani, ni maneno ya kututia moyo kabisa! Kama unamwamini Yesu, unaweza kusogea siku yako ya mwisho duniani ukiwa na kitu gani?  Ukiwa na moyo mkuu. Kama vile Charles Spurgeon alivyowahi kusema, “Usiogope kufa, mpendwa.  Kifo ni tukio la mwisho lakini ni tukio dogo ambalo Mkristo hatakiwi kufadhaishwa nalo.” 

Kama kweli unamwamini Yesu, hauna sababu ya kuogopa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.